Mashabiki wa Yanga, walimpokea Mkurugenzi wao wa Ufundi, Hans van der Pluijm kwa shangwe ya aina yake.
Pluijm aliingia na kukaa jukwaani VIP, lakini mashabiki walipomuona, walianza kumshangilia kwa nguvu hali iliyomlazimu kusimama na kuanza kuwapungia mkono.
Hali hiyo iliamsha shangwe na kuonyesha wengi wana mapenzi naye makubwa.
Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa naye aliungana naye kuwasalimia mashabiki hao ambao waliongeza shangwe hiyo.
Pluijm alikuwa kocha mkuu wa Yanga kabla ya mabadiliko na nafasi yake ikachukuliwa na George Lwandamina.
0 COMMENTS:
Post a Comment