February 26, 2017


Pamoja na kwamba Kocha Claudio Ranieri alionekana ameshindwa kabisa kuikomboa Leicester City kuporomoka daraja.

Taarifa zinasema uhusiano wa karibu kati ya wachezaji na mmiliki wa timu hiyo Vichai Srivaddhanaprabha ambaye ni mmiliki pia wa kampuni ya King Power pia ulichangia kufeli kwa kocha huyo.

Imeelezwa, baad ya Leicester kutwaa ubingwa wa England na kuwashitua watu wengi, kuanzia hapo Srivaddhanaprabha alianza kuwa na urafiki wa karibu na wachezaji.

Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wachezaji kuanza kupeleka maneno ya umbeya.

Lakini baadhi yao walianza kuonyesha wao ni wakubwa kuliko kocha kwa kuwa pia walikuwa na urafiki na mtoto wa mmiliki wa klabu hiyo.

Hali hiyo inaelezwa kuchangia kupunguza nidhamu na hofu kwa kocha na kusababisha kushuka kwa viwango vya wachezaji wengi.


Ingawa kila mmoja amekuwa hataki kulizungumzia na mzigo anaangushiwa kocha Ranieri kama ilivyo ada, lakini urafiki huo wa karibu wa Srivaddhanaprabha na wachezaji pia pamoja na mwanaye umeelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic