Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kuwa beki wa kati Mzimbabwe, Method Mwanjale, juzi alianza program ya mazoezi magumu na wenzake chini Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog.
Beki huyo alikuwa nje ya uwanja kwa wiki moja akiuguza majeraha ya enka aliyoyapata mechi ya Ligi Kuu Bara na Prisons kabla ya kutolewa nje kutibiwa.
Daktari Mkuu wa Simba, Yassin Gembe amesema tangu wameweka kambi Jumapili iliyopita beki huyo alikuwa ana program maalum ya binafsi kwa hofu ya kujitonyesha jeraha lake lakini tayari ameanza mazoezi magumu baada ya kumaliza program ya mazoezi mepesi ya binafsi.
Kaburu afunguka
Makamu mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ameweka wazi kwamba kikosi chao kipo kamili na kina matumaini makubwa ya kushinda mechi hiyo kwa sababu ya maandalizi ambayo wameyafanya.
0 COMMENTS:
Post a Comment