February 24, 2017Kikosi cha Simba, kikiwa kamili kimetua jijini Dar es Salaam, tayari kwa mechi ya kesho dhidi ya watani wao Yanga.

Simba walikuwa wameweka kambi mjini Zanzibar, sasa tayari wako jijini Dar es Salaam ambako wataweka kambi ya siku moja kabla ya mechi ya kesho.

Hata hivyo, Simba wamekuwa wagumu kutaja kambi watakayoweka jijini Dar es Salaam itakuwa wapi.

Hii imekuwa ni ile tabia ya hofu hasa inapofikia wakati wa mechi inayowakutanisha watani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV