February 15, 2017Baada ya kikosi cha Singida United kupanda ligi kuu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameahidi kufanyia marekebisho Uwanja wa Namfua, ambao utatumiwa na kikosi hicho kwenye michezo yake ya nyumbani.


Singida iliyo mikononi mwa kocha Fred Minziro ilipanda daraja wikiendi iliyopita kutoka kundi B baada ya kuwafunga wapinzani wao Alliance ya Mwanza.


Mwigulu amesema atalikamilisha suala la kuurekebisha uwanja huo kwa ajili ya kuufanya uwe kwenye mazingira mazuri kwa ajili ya kuwafanya Wanasingida wafurahie timu yao ikicheza hapo.

"Uwanja wa Namfua haupo vizuri na tunataka kuufanyia marekebisho tukishirikiana na wadau wa soka kwa ajili ya kuufanya uwe mzuri na wenye kuvutia.


"Lakini niipongeze Singida kwa juhudi walizofanya mpaka kupanda daraja lakini wanatakiwa kuendeleza pale walipoishia hili kuifanya timu ipate matokeo kwenye ligi kuu," alisema.Mwigulu ni miongoni mwa mawaziri kwenye serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV