February 26, 2017


Kiungo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema sababu kuu ya wao kupoteza, hawakuwa katika hamasa kuu.

Simba imeishinda Yanga kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara licha ya kwamba Yanga walitangulia kufunga bao katika dakika ya 5.


Niyonzima amesema kikosi chao hakikuwa kimehamasika kama ambavyo wenzao Simba ilikuwa.

“Walikuwa na hamasa ya juu, sisi mambo yalikuwa tofauti na huenda tulizidi kushuka kila mechi ilivyokuwa ikisonga mbele.

“Lakini nawapongeza Simba, kutoka nyuma, kusawazisha na kushinda. Si kitu kidogo hasa kwa timu kama Yanga ambayo imekamilika,” alisema.

Hata hivyo, Niyonzima hakutaka kufafanua kuhusiana na suala la hamasa.


Hata hivyo, tafsiri yake imezua kila aina ya gumzo wengine wakiamini hakukuwa na suala la ahadi au wachezaji hawakuwa na furaha wakati wa maandalizi yao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV