Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog aligundua jambo katika mwendo wa wachezaji wa Yanga, hali iliyomfanya ajiamini kwamba angeshinda licha ya kuwa walitangulia kupata bao katika dakika ya tano kupitia Simon MSuva.
Simba imeishinda Yanga kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini DAr es Salaam, jana.
Wakati wa mapumziko, Omog aliwaambia wachezaji wake kuendelea kushambulia kwa kasi licha ya kwamba Yanga wlaitangulia kufunga.
Aliwaambia wafanye hivyo kwa kuwa aliamini lazima kadiri kuda unayosonga mbele, Yanga wangechoka kwa kuwa hawakuwa na stamina ya kutosha.
"Kocha ndiye aliona, lakini hata baada ya kushambulia mfululizo, tulianza kuona Yanga kweli wamekuwa waoga.
"Kawaida mtu anapopoteza stamina, anachoka mapema na anapunguza hali ya kujiamini. Hivyo kocha aliona na sisi tukasikiliza maelezo yake," alisema Mohamed Zimbwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment