February 14, 2017


Pamoja na mwendo wa kusuasua, Ruvu Shooting wanaamini wana nafasi ya kubadilisha mambo na kukaa vizuri.

Msemaji wa Shooting, Masau Bwire amesema imani yao wanapita katika mawimbi tu.

"Sasa tunapita katika upepo na mawimbi makali. Lakini siku chache tutakaa vizuri na kufanya vizuri.

"Kama nilivyosema mwanzo, soka lao ni bora na la kuuvtia. Lakini tumekuwa hatufungi mabao, lakini utaona," alisema.

Mwendo wa Ruvu Shooting umekuwa wa kusuasua katika Ligi Kuu Bara ambayo wamerejea msimu huu baada ya kuteremka msimu mmoja kabla.

Hali hiyo imesababisha kuanza kuonekana kama wasipokuwa makini, "Safari itawakuta" kurejea Ligi Daraja la Kwanza.

Lakini Masau Bwire amekuwa akikataa katakata na kusisitiza wana nafasi ya kurejesha nguvu yao na kujikomboa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV