February 24, 2017


KULIA NI JENGO AMBALO YANGA WAMEWEKA KAMBI YAO YA SIKU MBILI, KUSHOTO LINAONEKANA JENGO LA JUBILEE TOWER AMBAKO OFISI ZA MOHAMMED DEWJI ZIKO HAPO.

Wakati watani wao Simba wamerejea kutoka Zanzibar na kujichimbia mitaa ya Mbezi Beach, Yanga wameamua kubaki katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Yanga itakuwa na kibarua cha kuwavaa Simba katika mechi ya pili ya Ligi Kuu Bara baina ya timu hizo kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Yanga ilikuwa kambini Bagamoyo lakini sasa imerejea na kujichimbia katika hoteli hiyo karibu kabisa zilipo Ofisi za Mohammed Dewji.

Dewji ambaye amekuwa akiisaidia Simba katika suala la kulipa mshahara, lakini pia ametangaza nia ya kununua hisa asilimia 51, ofisi zake ziko katika jengo la Jubilee Tower, hatua 100 tu hadi ilipo hoteli hiyo ya kisasa.


Yanga itatokea hapo kwenda Uwanja wa Taifa kesho, tayari kuwavaa Simba.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, watani hao walimaliza mchezo kwa sare ya bao 1-1 huku Simba wakilazimika kusawazisha mwishoni kwa bao la Shiza Kichuya aliyechonga mkwaju wa kona ukatinga moja kwa moja wavuni.


Ramada Encore ni moja ya hoteli mpya za kisasa zilizo katikati ya jiji la Dar es Salaam enero lijulikanalo kama Posta.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV