February 11, 2017



Mazoezi ya Yanga, jana asubuhi yalipooza na kabla ya kuanza kwake wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi walionekana kuwa na shauku ya maendeleo ya mwenyekiti wao, Yusuf Manji anayeshikiliwa katika Kituo cha Kati cha Polisi ‘Central’ jijini Dar es Salaam.


Juzi Manji alijisalimisha central kwa ajili ya mahojiano kuhusu dawa za kulevya kama alivyotakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, hadi jana jioni mwenyekiti huyo alikuwa anashikiliwa na polisi.


Katika mazoezi ya Yanga, jana asubuhi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, baadhi ya wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi walionekana kutokuwa na furaha ya siku zote.


Baadhi ya watu wa benchi la ufundi walikuwa wakiuliza kwa waandishi wetu kuhusu Manji kama alilala polisi au alirudi nyumbani kwake na wengine kusema wazi kwamba hali itakuwaje kama akiendelea kuwa ndani.


“Manji ndiye kila kitu kwetu, anatoa fedha nyingi kwa klabu sasa kama akibaki ndani sijui hii safari yetu ya Comoro itakuwaje, kwani ajatolewa bado?” alihoji mmoja wa wachezaji waandamizi wa timu hiyo.


Kiongozi mmoja wa benchi la ufundi alisema: “Mpaka sasa hatujui mwenyekiti wetu amelala wapi baada ya kwenda kituoni, kama hawatamuachia na sisi safari yetu sijui itakuaje kwani yeye ndiye kila kitu.”



Hata hivyo, jana mchana Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amehakikisha kuwa, taratibu zote za timu kuondoka zipo sawa na leo alfajiri msafara wa watu 30 ungeondoka kwenda Comoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic