February 25, 2017



Rekodi hazidanganyi kwani hadi sasa ni wachezaji watatu tu walioweza kufunga mfululizo katika mechi tatu za watani wa jadi Simba na Yanga.

Wachezaji hao ni Kitwana Manara wa Yanga ambaye ni baba mdogo wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, Madaraka Selemani wa Simba na Amissi Tambwe wa Yanga.

Sasa ishu ipo hivi, ni Tambwe pekee anayeweza kuvunja rekodi ya kufunga mara ya nne mfululizo katika mechi hiyo ya watani wa jadi kwani leo anaweza kuichezea Yanga dhidi ya Simba.

Kitwana Manara na Madaraka wote wameshaachana na soka la ushindani, hivyo nafasi ipo kwa Tambwe, raia wa Burundi leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara.

Tambwe alianza kuifunga Simba Septemba 26, 2015 (Simba 0-2 Yanga), Februari 20, 2016 (Yanga 2-0 Simba) na Oktoba Mosi, 2016 ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Katika mechi zote hizo, Tambwe alifunga bao moja moja.
Kitwana Manara

Machi 30, 1968 (Yanga 1-0 Sunderland)
Juni Mosi, 1968 (Yanga 5-0 Sunderland)
Juni 04, 1972 (Yanga 1-1 Simba)

Madaraka Selemani
Julai 2, 1994 (Simba 4-1 Yanga)
Nov. 2, 1994 (Simba 1-0 Yanga)

Nov. 21, 1994 (Simba 2-0 Yanga)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic