February 10, 2017Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga amefika katika kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dar es Salaam kwa tuhuma za suala la madawa ya kulevya zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


Sanga alifika kituoni hapo na kupitiliza moja kwa moja lango la ukaguzi na baadaye alienda lango kuu la kuingilia ndani.

Haijajulikana mara moja, alikuwa akifanya nini zaidi ni kwenda kumuona mwenyekiti wake anayeshikiliwa tokea jana.


Baada ya kutoka, Sanga hakutaka kuzungumza lolote lakini imeelezwa amekuwa akishughulikia masuala kadhaa ya kisheria pia kuhakikisha timu inasafiri kwenda Comoro kwa kuwa Manji ambaye ni kiongozi mkuu yuko mahabusu na yeye ndiye hushughulikia masuala ya fedha hasa suala la uidhinishaji.


“Sanga alikwenda kumjulia hali Manji. Lakini lazima watakuwa wamejadili masuala ya klabu. Hawezi kuyazungumzia hayo hadharani,” kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV