March 11, 2017Yanga inatarajiwa kuvaana na Zanaco ya Zambia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya Azam Media imemwaga kitita cha Sh milioni 35 ili kuonyesha mchezo huo mubashara.

Taarifa za ndani zinaeleza, Azam TV itaonyesha mechi hiyo moja kwa moja kutoka Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Kweli limetika fungu hilo na mechi itaonyeshwa moja kwa moja," kilieleza chanzo.


Hata hivyo, mambo yamekuwa yakienda chinichini ili kuhakikisha wengi wanajitokeza uwanjani na kuishangilia Yanga.

Siku nne zilizopita, Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amekuwa akisisitiza na kuwaomba mashabiki kwenda kuishangilia Yanga.

Huo ni mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambapo mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi na atakayeondolewa kwenye hatua hii, atashushwa Kombe la Shirikisho ambako atatakiwa kucheza mechi mbili za mtoano kabla ya kutinga makundi.

Yanga iliiondoa N’gaya ya Comoro kwenye hatua ya awali kwa mabao 6-2 na Zanaco ya Zambia iliiondosha APR ya Rwanda kwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV