March 11, 2017

KESSY


Leo Jumamosi Yanga inatarajiwa kuvaana na Zanaco ya Zambia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, lakini Straika wa Simba, Juma Liuzio, amempa beki wa Yanga, Hassan Kessy jina la mchezaji hatari wa wapinzani wao.


Huu ni mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambapo mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi na atakayeondolewa kwenye hatua hii, atashushwa Kombe la Shirikisho ambako atatakiwa kucheza mechi mbili za mtoano kabla ya kutinga makundi.

LIUZIO

Ikumbukwe Yanga iliiondoa N’gaya ya Comoro kwenye hatua ya awali kwa mabao 6-2 na Zanaco ya Zambia iliiondosha APR ya Rwanda kwa bao 1-0.


Liuzio ambaye amewahi kuchezea Zesco ambao ni wapinzani wa Zanaco, amemtaja beki Mzimbabwe, Zimiseleni Moyo ‘Rasta’ kuwa ndiye amekuwa mwiba kwa kuanzisha mashambulizi kupitia upande wao wa kulia na kukaba kwa wakati mmoja.


"Ule upande wa kulia, Kessy inabidi acheze kwa umakini mkubwa kwa sababu Zanaco hutumia upande wao wa kushoto kutengeneza mashambulizi yote na hata mabao yao hupatikana huko.


"Nimwambie kwamba, macho na akili yake inatakiwa ielekezwe zaidi kwa Moyo ambaye yeye ni beki lakini hatari sana," alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV