Wanachama wa Simba mkoani Kagera wameanza maandalizi ya kukipokea kikosi chao.
Simba itasafiri wikiendi hii kwenda Bukoba kwa ajili ya kuivaa Kagera Sugar katika mechi inayotarajiwa kuwa kali.
Wanachama wa Simba, tawi la Kichwabuta, wameamua kuanza maandalizi mapema.
Moja ya jambo ambalo wamelifanya ni vikao kadhaa vya maandalizi hayo ili kuhakikisha Simba wanaona wako nyumbani.
Kama haitoshi, majengo ya tawi lao, yamefanyiwa ukarabati ikiwa ni pamoja na kupakwa rangi ili Simba wakitua, wawe na amani na wenye ari ili kushinda mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment