March 25, 2017Kiungo mkongwe wa Yanga, Thabani Kamusoko, raia wa Zimbabwe, amesema kikosi chao hicho kitaweka historia kwa kuitoa MC Alger ya Algeria na kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga imepangwa kucheza mtoano na Waarabu hao baada ya kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Zanaco ya Zambia. Yanga haina rekodi nzuri inapocheza na timu za Afrika Kaskazini.

Kiungo huyo aliyefunga mabao matano msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara, aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram kuwa; “Ratiba ndiyo hii, twendeni tukapambane na huu ndiyo muda wetu wa kuhakikisha tunatinga hatua ya makundi, twendeni tukapambane ili kuandika historia kwa mara nyingine.”

Kamusoko katika andiko lake aliwataja wachezaji wenzake kama Donald Ngoma, Simon Msuva, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke akiwataka wapambane kuwatoa Waarabu.


Michezo ya kwanza ya hatua hiyo inatarajiwa kupigwa kati ya Aprili 7 hadi 9, mwaka huu huku mechi za marudiano zikipigwa wiki moja baadaye.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV