March 14, 2017

Mshambuliaji Donald Ngoma, sasa uhakika hatasafiri na kikosi cha Yanga kwenda Zambia.

Ngoma ambaye alirejea uwanjani katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco ya Zambia, aliumia na kutolewa.

Habari za ndani kutoka Yanga, zinaelezwa tayari ameondolewa katika majina ya wachezaji wanaokwenda Zambia keshokutwa Alhamisi.

“Ngoma kaumia, tayari amerejea katika matibabu tena,” kilieleza chanzo.

“Sijui, labda kuangalia kama nafuu inawezekana. Lakini alivyo hakuna matumaini ya kucheza sasa tena.

“Inawezekana akaendelea kukaa nje kwa kipindi kirefu.”


Awali Ngoma alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kabla ya kurejea na kuumia tena.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV