March 14, 2017Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga wanatarajia kuondoka nchini keshokutwa kwenda Zambia.

Yanga wanakwenda Lusaka katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zanaco Jumamosi, baada ya sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga watakwenda Zambia kupitia Nairobi, Kenya wakitumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya maarufu kama KQ.

Kawaida, KQ hutumia ndege aina ya Boieng 777 kwenda mjini Lusaka na baadaye Afrika Kusini. Lakini kutoka Dar hadi Nairobi hutumia ndege ndogo au Boieng 737.

Awali ilielezwa kwamba Yanga wangetumia Treni ya Tazara kwenda Zambia, jambo ambalo baadaye lilikanushwa na uongozi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV