March 16, 2017



Fifa imetangaza kuifungia nchi ya Mali kushiriki michuano ya kimataifa kwa madai ya serikali kuingilia masuala ya soka.


Waziri wa Michezo wa Mali, Housseini Amion Guindo aliamua kuunda kamati ya muda kuendesha Shirikisho la Soka la Mali (Femafoot) baada ya kuona uongozi uliokuwa madarakani kutokuwa sahihi.

Lakini baada ya Femafoot kufikisha malalamiko yake Fifa, shirikisho hilo la soka la limataifa, likaiamuru serikali ya Mali, kuvunja kamati hiyo hadi Ijumaa.

Baada ya kuona hakukuwa na utekelezaji hadi leo usiku huku zikiwa zimebaki saw chache kabla ya muda kufika, Fifa imetangaza kuifungia Mali.

BARUA YA FIFA KWENDA FEMAFOOT


Katibu Mkuu wa Fifa, Fatma Samoura alisisitiza serikali ya Mali kuachana na kuingilia michezo na kutaka Rais wa Femafoot, Boubacar Baba Diarra aachwe aendelee kuongoza.

Mwisho, Fatma Samoura ndiye aliyeandika barua hiyo ya kuifungia Mali kushiriki michuano iliyo chino yake, mambo ambalo bila shaka ni pogo kwa Mali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic