March 16, 2017
Mbwana Samatta ameweka rekodi nyingine kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya Europa League hatua ya robo fainali.

Samatta ameweka rekodi hiyo baada ya timu yake ya KRC Genk kufuzu baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya pili ya hatua ya 16 Bora, leo.

Katika mechi ya kwanza, ikiwa ugenini, Genk iliibabua Gent kwa mabao 5-2 ikiwa kwake. Samatta alitupia mawili.


Sare ya 1-1, maana yake Genk inakwenda robo fainali kwa jumla ya mabao 6-3.

Kabla, Samatta alikuwa ameandika rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya Europa hatua ya 16 bora.

Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe ya DR Congo aliyoiwezesha kubeba makombe lukuki likiwemo la ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV