March 16, 2017
KRC Genk ya Ubelgiji anayoichezea Mtanzania Mbwana Samatta imefuzu kucheza hatua ya robo fainali katika Europa League.

Genk imefuzu baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya pili ya hatua ya 16 Bora, leo.

Katika mechi ya kwanza, ikiwa ugenini, Genk iliibabua Gent kwa mabao 5-2 ikiwa kwake. Samatta alitupia mawili.Sare ya 1-1, maana yake Genk inakwenda robo fainali kwa jumla ya mabao 6-3.

Samara alicheza kwa dakika zote 90 na Genk ilipata bao lake kupitia Timothy Castagne katika dakika ya 20. Bao likadumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza.


Kipindi cha pili ilikuwa ni vita nikuvute na Gent wakapata bao la kusawazisha katika dakika ya 84 kupitia Louis Vertstrate. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV