March 23, 2017Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, mapema leo ametinga katika studio za EFM na TVE, kwa ajili ya kumpa pole Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho, Majay kutokana na matatizo yaliyomkuta ya kutuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya.

Akizungumza na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa EFM na TVE, Gwajima alisema kuwa, lengo kuu la yeye kutembelea hapo ni kuwatia moyo kutokana na matatizo hayo yaliyompata mkurugenzi wao.


“Nipo hapa kwa ajili ya kuwatia moyo na kikubwa niwaambie tu kuwa Mungu yu pamoja nanyi, hivyo msikatishwe tamaa na mtu au jambo lolote lile kwani hakuna jaribu lisilokuwa na suluhisho lake.


“Kikubwa zaidi nawaomba mjuwe tu kuwa kila baya linapotokea basi amini mbele yake kuna neema ya bwana inakuja, niwapongeze kwa kuwa na umoja na ushirikiano ambao hata mimi mmenionyesha wazi lakini kikubwa nitaendelea kuwaombea ili Mungu awaongezee ili muweze kuajiri watu wengi zaidi,” alisema Gwajima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV