March 9, 2017Kikosi cha KRC Genk kianshuka dimbani leo katika mechi ya Europa Cup dhidi ya KAA Gent pia ya Ubelgiji.

Mechi hiyo itakuwa na upinzani mkali huku Mtanzania, Mbwana Samatta akitarajiwa kuongoza safu ya ushambulizi.

Samatta ambaye ana mabao 14 baada ya kuichezea Genk kwa mechi 43, ndiye tegemeo la ushambulizi la timu hiyo.

Genk itakuwa ugenini ikitegemea kumaliza kazi ili kusonga mbele katika michuano ya Europa.

Beki wa kati wa Simba, Juuko Murshid yuko fiti kucheza mechi zinazofuatia za Simba.

Juuko alirejea nchini kuungana na Simba baada ya kuumia kwa Method Mwanjale.

Hata hivyo, aliomba kupewa muda kidogo ili kurejesha hali ya ubora sahihi.

Lakini imeelezwa sasa yuko tayari kuitumikia Simba katika mechi zinazofuata.

“Unaweza kusema yuko fiti, ukiangalia mazoezi amefanya kwa muda wa kutosha na suala la acheze au asicheze mechi linabaki kwa mwalimu mwenyewe,” alisema Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi.


Simba ililazimika kumtumia kiungo mkabaji James Kotei katika nafasi ya beki wa kati kutokana na kuumia kwa Mwanjale na Novaty Lufunga na Besala Boukungu kuwa na adhabu ya kadi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV