March 9, 2017
Kikosi cha KRC Genk kianshuka dimbani leo katika mechi ya Europa Cup dhidi ya KAA Gent pia ya Ubelgiji.

Mechi hiyo itakuwa na upinzani mkali huku Mtanzania, Mbwana Samatta akitarajiwa kuongoza safu ya ushambulizi.

Samatta ambaye ana mabao 14 baada ya kuichezea Genk kwa mechi 43, ndiye tegemeo la ushambulizi la timu hiyo.

Genk itakuwa ugenini ikitegemea kumaliza kazi ili kusonga mbele katika michuano ya Europa.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV