March 25, 2017




Na Saleh Ally
MTANZANIA Mbwana Samatta ni mfano wa kuigwa na anaweza kuwa chachu ya mafanikio kwa vijana wengi hasa wale wenye umri chini yake ambao vizuri wakifikiri wanataka kuwa au zaidi yake.

Mimi kutoka moyoni, namuona Samatta ni kijana Mtanzania kati ya wachache sana ambao wamekuwa na tamaa ya mafanikio bila kujali wanatokea kwenye familia yenye uwezo wa chini au kawaida.

Huenda, raha ingekuwa kufikiria ametokea katika familia ya kawaida au masikini lakini leo amefikia alipo.

Yeye binafsi, anaonekana si mtu mwenye majivuno na huenda anayechukia hata kutangazwa ana uwezo wa kitu fulani hata kama ni ukweli. Hatuwezi kumuona mbaya kwa kuwa hii ni hulka yake, tuheshimu hili, inapobidi.

Lakini vizuri kumuangalia kama sehemu ya darasa na ikiwezekana kumtumia vizuri kuwahamasisha vijana wetu wengine zaidi na zaidi kumfikia alipo, wampite na mwisho Tanzania iwe na mafanikio zaidi na zaidi.

Sidhani kama huu ni wakati mwafaka wa kuanza kujadili eti Samatta amevaa viatu vya aina gani. Hii ni kupoteza muda!
Viatu vya kuchezea soka anavyovaa Samatta, wengi sana hawawezi kushindwa kununua. Saleh Ally naye  anaweza kununua kwa wingi tu.

Lakini bado ninaona viatu si jambo muhimu sana. Siwezi kuzuia mijadala yote au kuwapangia watu. Lakini ninaweza kushauri kwa kile ambacho ninaona ni bora.

Moyo wa uamuzi wa Samatta kukataa kwenda kuichezea Simba baada ya kulaghaiwa, na bado akafanikiwa, anao nani mwingine?

Moyo wa kuonyesha kipaji cha juu na kuipandisha Mbagala Market katika Ligi Kuu Bara huku akiwa mfungaji bora na mchezaji bora wa timu, nani anaweza?


Akili na uwezo wa kupambana akiwa DR Congo, katika timu kubwa na bora kama TP Mazembe na akafanikiwa ikiwa ni pamoja na kubeba ubingwa wa Afrika, kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika, nani ameweza?


Viatu ni vitu vidogo sana. Sidhani kama tunaweza kuwasaidia vijana wetu kuona umuhimu wa Samatta kwa kujadili anavaa nini.

Mimi na wewe, tunaweza kuwa sehemu ya msaada na kuwasaidia Watanzania wanaochipukia katika michezo kupitia Samatta. Tumtumie vizuri kuzalisha na kuendeleza zaidi vipaji vya vijana wetu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic