March 10, 2017





Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeagiza sekretarieti ya TFF kutoa wito mwingine kwa wanafamilia watatu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) walioshitakiwa mbele ya kamati hiyo.


Walioshitakiwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ni Mwenyekiti wa RUREFA, Blassy Kiondo; Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, James Makwinya na Kaimu Katibu Mkuu wa RUREFA, Ayoub Nyaulingo.


Madai dhidi ya wanafamilia hao wa mpira wa miguu ni kudharau maagizo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF ya kuwataka wasimamishe mchakato wa uchaguzi wa Mkoa mpaka rufaa zilizowasilishwa TFF zitakaposikilizwa.


TFF ilipeleka mwito wa kuwataka watuhumiwa hao kwenda kujibu madai hayo mbele ya Kamati ya Nidhamu, Machi 8, mwaka huu lakini watuhumiwa hawakutokea kwa sababu mbalimbali.


Lakini Kamati kwa kuzingatia kanuni ya Nidhamu iliona ni vyema watuhumiwa wakapata nafasi tena ya kuja kujitetea mbele ya kamati hiyo na kama ikitokea wameshindwa kufika, basi watume wawakilishi wao au utetezi kwa njia ya maandishi katika kikao kingine kitakachofanyika Machi 15, mwaka huu saa 12.00 jioni kama barua inavyojieleza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic