Yule shabiki wa Yanga, Kanjunju John ‘aliyebeti’ Sh 50,000 na kuliwa, kumbe aliweka pia simu yake mkononi akitamba timu yake itashinda lakini akaliwa baada ya kufungwa mabao 2-1 na Simba.
Kanjunju aliyejitambulisha kama mkazi wa Jangwani jijini Dar es Salam, amejizolea umaarufu baada ya video yake kusambaa mitandaoni akionekana analia kutokana na Yanga kufungwa na Simba.
Wakati akilia, Kanjunju alikuwa akisisitiza kupoteza Sh 50,000 alizobeti kwamba Yanga itashinda lakini akazipoteza kwakuwa timu hiyo ilifungwa, alisema fedha hizo zilikuwa za mtaji wake wa biashara.
Tulika eneo la biashara la Kanjunju, Karume jijini Dar es Salaam na kumkuta mmoja wa rafiki zake ambaye alisema; “Kanjunju siku hizi hana simu kwani nayo aliliwa alipobeti Yanga itashinda.
“Mtaji pia hana na hapa tunampa mali kwa mali kauli kwamba akiuza ndiyo analeta fedha na sasa ameshaenda katika biashara zake. Sasa anasema anatafuta nauli ili Jumapili aende Morogoro kutazama mechi ya Yanga na Mtibwa Sugar.”
Tayari Yanga kupitia kwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Salum Mkemi ilikuwa ikimtafuta Kanjunju ili imrejeshee Sh 50,000 alizopoteza baada ya timu yake kufungwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment