March 1, 2017




Baada ya kikosi ca Azam kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), kocha mkuu wa timu hiyo, Mromania, Aristica Cioaba, ameweka bayana kwamba wamewekeza nguvu kubwa kuhakikisha wanautwaa ubingwa wa kombe hilo kutokana na ubingwa wa ligi kuwa ngumu kuutwaa.


Azam imetinga hatua hiyo baada ya kuiondosha Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa bao 1-0, katika mechi iliyopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar.


Timu nyingine zilizotinga hatua hiyo ni Simba, Madini FC ya Arusha na Kagera Sugar, Ndanda, Mbao na Prisons huku wakisubiria mchezo kati ya Yanga na Kiluvya ya Pwani.


Cioaba amesema ameamua kuwekeza mawazo yake kwenye kombe hilo kwa ajili ya kujitengenezea nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kama ambavyo wamekuwa wakishiriki kwa muda mrefu.


“Hatuna nafasi kwenye ligi kusema kwamba tutatwaa ubingwa kwa sababu waliopo juu yetu wamekuwa wakifanya vizuri labda nafasi ya pili japo kwenye soka chochote kinatokea lakini hatuwezi kukata tamaa tutaendelea kupigana hadi mwisho wa msimu.


“Lakini huku FA tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri ikiwezekana kutwaa ubingwa na tutahakikisha tunatumia nguvu kwa kiasi kikubwa kuweza kutwaa ubingwa wa kombe hilo hili tupate nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa,” alisema Cioaba.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic