March 1, 2017


Straika wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameweka wazi sababu iliyomfanya ashindwe kufanya vizuri katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, lakini pia amewapongeza Simba.

Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa Simba iliitandika Yanga mabao 2-1, na kufanikiwa kujikita juu kabisa kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 54 na kuiacha Yanga nafasi ya pili ikiwa na pointi 49.

Tambwe ambaye tangu ajiunge na Yanga amekuwa akiionea Simba kwa kuifunga alisema kuwa katika mechi hiyo hakuwa na bahati kwani alijitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha anapata bao lolote lakini mambo yalikuwa magumu.

“Mechi ilinikataa siku hiyo hivyo ndivyo ninavyoweza kusema, hakuna jambo lingine lakini nilijitahidi sana kupambana vilivyo ila mambo hayakuwa mazuri.
“Hata hivyo, niwapongeze tu Simba kwa ushindi huo waliupata na sisi tuliyakubali matokeo hayo kwani siku zote mchezo wa soka ndivyo hivyo,” alisema Tambwe.


Katika mchezo wa mzuguko wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 huku bao la Yanga likifungwa na Tambwe na Simba likifungwa na Shiza Kichuya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV