March 19, 2017
Mchezo umemalizika: Simba imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Madini FC.
 
Dakika ya 90 + 4: Mchezo unaweza kumalizika muda wowote kutoka sasa.
 
Dakika 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika nne za nyongeza.
 
Dakika ya 90: Mchezo unaelekea kumalizika na timu zote zinashambuliana kwa zamu.
 
Dakika ya 85: Kiungo wa Simba, Kotei yupo chini, ameumia baada ya kugongana na mchezaji wa Madini.

 Dakika ya 80: Bila shaka Madini wameonyesha ukomavu kwa kutoa upinzani mzuri kwa Simba. Mchezo unaendelea na unachezwa zaidi katikati ya uwanja.
 
Dakika ya 76: Timu zote zinacheza soka la kasi.

Dakika ya 71: Kasi ya mchezo imeongezeka kwa pande zote.

Dakika ya 68: Kichuya anakosa nafasi ya wazi, anabaki na kipa lakini kipa anafanya kazi nzuri kuokoa.
 
Dakika ya 63: Madini wanafanya shambulizi kali, lakini shuti linalopigwa kutoka nje ya eneo la 18 linapaa juu ya lango la Simba.

Dakika ya 60: Madini FC wanaonyesha upinzani kwa kujibu mashambulizi kwa Simba.
 
Dakika ya 54: Simba wanapata bao kupitia kwa Laudit Mavugo, anafunga kwa kichwa baada ya beki wa Madini kujichanganya katika kuuzuia mpira huku kipa wake akiwa amesogea mbele ya lango lake.
 
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 54: Simba wanaongeza mashambulizi katika lango la Madini.

Dakika ya 46: Ajibu anapata nafasi lakini anashindwa kuitumia akiwa karibu na lango la Madini.

 Mchezo umeanza.
 
Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza kipindi cha pili.
 
MAPUMZIKO
 
Dakika 45: Kipindi cha kwanza kimekamilika.
 
Dakika 45: Mwamuzi anajiandaa kupuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza.

Dakika ya 42: Mchezo bado wanashambuliana kwa zamu.
 
Dakika ya 36: Kiungo wa Simba, Mzamiru Yasin apataka kadi ya njano kutokana na kuonyesha mchezo mbaya.
 
Dakika ya 30: Simba wanafanya shambulizi kali, Ibrahim Ajibu anapiga shuti kali kutoka nje ya 18, mpira uangonga mwamba na kurejea uwanjan.
 
Dakika ya 24: Beki wa kati wa Simba, Juuko Murshid anapata kadi ya njano kwa kumchezea vibaya mchezaji wa Madini.
 
Dakika ya 19: Madini wanashindwa kutumia nafasi wanayoipata kufunga bao, kumetokea piga nikupige katika lango la Simba lakini walinzi wa Simba wakaokoa.
 
Dakika 14: Simba wanapata kona, anapiga kona Kiochuya lakini inashindwa kuwa na faida kutokana na walinzi wa Madini kuokoa.

Dakika ya 7: Matokeo bado ni 0-0, idadi ya mashabiki ni wengi hapa uwanjani.

Dakika ya 5: Timu zote bado zinasomana na kasi ya mchezo haijawa kubwa.

Dakika ya 1: Mchezo umeshaanza

Kikosi cha Simba ambacho kimeanza katika mchezo wa leo ni hiki hapa, chini ya Kocha Joseph Omog, ni mchezo wa Kombe la Shirikisho:

KIKOSI:
1. Daniel Agyei
2. Besala Bukungu
3. Mohamed Zimbwe 
4. Abdi Banda
5. Juuko Murshid 
6. James Kotei
7. Shiza Kichuya
8. Mzamiru Yassin
9. Laudit Mavugo
10. Ibrahim Ajibu
11. Mohamed Ibrahim

AKIBA:
Peter Manyika
Hamadi Juma
Vincent
Said Ndemla
Juma Luizio
Jonas Mkude
Athanas Pastory

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV