March 19, 2017



Wakiwa nyumbani, Mbabane Swallows wameonyesha ni watu wengine kabisa baada ya kuichapa Azam FC kwa mabao 3-0.

Katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho jijini Dar es Salaam, Azam FC ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’.

Hii maana yake, Azam FC wameng’olewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kuchapwa jumla ya mabao 3-1.

Katika mechi hiyo ya leo mjini Mbabbane, Swaziland, wenyeji walionekana kutawala muda mwingi na mashambulizi yao yalikuwa makali zaidi.


Mara kadhaa, Azam FC ilijitahidi kutengeneza nafasi lakini kulikuwa na udhaifu katika kuzitumia ili kusaidia kupatikana kwa matunda.

3 COMMENTS:

  1. hongereni sana watanzania kwa uhodari wenu wa kuwapongeza akina Bakhresa hata wanapoifunga timu dhaifu moja bila na kuikandya Yanga kila wakati na kuizomea inapocheza nyumbani. Anayepanda upepo huvuna dhoruba!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mi naipongeza Yanga kwa kuitoa kwa taabu sana timu ngumu ya Comoros, Ngaya. Yanga vidume bwaanaaa

      Delete
  2. Azam ilistahili kabisa kutolewa ksani hadi goli la Dar, lilikuwa la off side ya wazi kabisa na ilionekana wazi kuwa Azam isingeweza kuimudu Mbabane Swallows kwao. Azam bado kuna tatizo kubwa la kiufundi, kwani hata shule sio majengo mazuri, bali ni vifaa vya kufundishia na kujifunzia, walimu wazuri na watoto wenye nidhamu. Azam wana pesa lakini hawana vision. Wanakurupuka sana. Hakukuwa na sababu ya kumuacha kocha kama Stewart Hall au Omog waliyekaa naye msimu mmoja tu. Sasa wamesajili wachezaji kibao toka nchi moja na kuajiri kocha toka Romania! Walitumia vigezo gani? John Bocco ambaye wameng'ang'ana naye miaka mingi wangempima kwa ubora wake akiwa timu ya Taifa na sio kwa kuzifunga tu Simba na Yanga. John Bocco keshawahi kufunga hata goli moja timu ya taifa, licha kuitwa mara kibao kuichezea Taifa Stars? Kingine kinachoiponza Azam ni kusahau kuwa 'imezaliwa' kutoka Simba, maana kina Bakhressa, ndio hao hao walikuwa wafadhili wa Simba miaka ya nyuma. Hivyo Azam kujiona imekua, kiasi cha kusahau ilikotoka, ni kupotoka. Ingeutumia 'udugu' wake na Simba vizuri, ingeweza 'kuchomoza' kimataifa, maana ni Simba pekee nchi hii, ndiyo ambayo inashikilia rekodi ya kufanya vizuri kimataifa. Wengine ni 'washiriki' tu, na sio washindani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic