March 31, 2017


Yanga wamekuwa na hofu kubwa kutokana na suala la majeruha kuwaandama.


Mshambuliaji Donald Ngoma bado anaonekana hana nafasi ya kuisaidia Yanga katika mechi dhidi ya Azam FC, kesho.

Ngoma anaonekana hajapona vizuri hali inayosababisha hofu kubwa kwa Yanga ambayo italazimika kuwategemea Obrey Chirwa na Simon Msuva.

Mshambuliaji mwingine, Amissi Tambwe naye ni majeruhi, hivyo kumfanya Kocha George Lwandamina kuwa na wakati mgumu.

Katika mazoezi ya leo, Ngoma alionekana hakuwa vizuri hali inayoashiria kama hakufanya kitu leo, basi kesho ana nafasi ya asilimia chache kucheza.

Kama Yanga itapoteza mechi ya kesho dhidi ya Azam FC itakuwa imejiweka katika wakati mgumu sana.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV