March 22, 2017


Mashabiki wa soka hawaishi vituko. Leo wamekuwa wakitupia picha za kiungo wa Chelsea, Ng’olo Kante kwamba wakati watu wanasema asilimia 70 ya dunia ni maji, basi sehemu iliyobaki ni mali ya Kante.

Mashabiki hao wanaamini Kante ndiye kiungo bora hasa katika ukabaji katika kipindi hiki.

Utani huo umefika mbali zaidi kuwa kama ni bahari, basi bahari Kante ina kina kirefu zaidi kuliko mengine yote.


Kante amezidi kupata umaarufu baada ya kuingoza Chelsea katika mbio za kubeba ubingwa huku ikionekana Leicester City ambao ni mabingwa watetezi wa England, kuonekana wanayumba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV