March 22, 2017Azam FC wamesema kweli hawakutendewa haki nje ya uwanja walipokuwa Swaziland ambako walifungwa kwa mabao 3-0 dhidi ya Mbabane Swallows na kung’olewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Lakini wamekiri kwamba, waamuzi walikuwa hawana tatizo na waliwachezesha kwa haki.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema walikuwa na wakati mgumu sana nje ya uwanja.

“Polisi wanaonekana walipangwa, walitushambulia. Kama haitoshi, vyumba vilipuliziwa dawa na tukalazimika kuwapeleka wachezaji wavalie kwenye gari.

“Hii iliwaumiza kisaikolojia. Lakini kwa upande wa waamuzi, walikuwa fair na nafasi tulipata lakini hatukuzitumia,” alisema.

Ushindi wa mabao 3-0 uliitoa Azam FC kwa jumla ya mabao 3-1 kwa kuwa ilishinda 1-0 katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV