Mashabiki wa Yanga, Jumamosi iliyopita walishindwa kuzizuia hasia zao baada ya timu hiyo kufungwa na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kumtaka kocha wao mkuu, Mzambia George Lwandamina awaambie sababu zilizomfanya amsajili, Mzambia mwezake, Justine Zulu.
Mashabiki wao ambao walikuwa wamefura kwa hasira walimvamia Lwandamina wakati alipokuwa akitoka katika vyumba vya kubadilishia nguo uwanjani hapo na kwenda kupanda gari ambapo walimtaka awaambie ni sababu zipi zilizomfanya amsajili Zulu akijua kabisa siyo aina ya mchezaji ambaye walikuwa wakimhitaji.
“Tunashukuru kocha kwa usajili wao wa Zulu ulioufanya kwani tumeona mchango wake katika kikosi chetu, lakini unaweza kutuambia ni sifa zipi zilizofanya ukamsajili.
“Sisi tulikuwa hatutaki mtu wa kupiga pasi tu isipokuwa tulikuwa tunataka mtu mwenye uwezo wa kukaba na siyo wa kupiga pasi tu kama alivyo Zulu, ni bora ungetuachia Mbuyu Twite,” walisikika mashabiki hao wakimwambia Lwandamina ambaye hakuwajibu chochote na kuondoka.
Zulu ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Zesco mwezi Desemba mwaka jana, ameshindwa kukata umeme kama ilivyokuwa ikitarajiwa na wengi.
Usajili wa Zulu ndiyo pekee alioufanya kocha huyo tokea ajiunge na Yanga huku akimruhusu Mkongomani, Mbuyu Twite aende zake.
0 COMMENTS:
Post a Comment