March 1, 2017



Straika wa Simba, Laudit Mavugo ameibuka na kusema kuwa siri ya mafanikio ya kufumania nyavu hivi karibuni na kwenye mechi ya Yanga kunatokana na bibi yake aliyekuwa Bunjumbura, Burundi kumsapoti na kumuombea kila siku.

Mavugo amekuwa na wakati mgumu wa kufumania nyavu tangu alipotua katika kikosi hicho cha Msimbazi, lakini siku za hivi karibuni ameonekana kuamka upya.

Katika mchezo wa wikiendi iliyopita kati ya Yanga na Simba Mavugo alifanikiwa kufunga bao lake la saba kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu wakati alipoiongoza Simba kupata ushindi wa mabao 2-1.


Mavugo amesema kuwa, amekuwa katika wakati mgumu wa kuweza kufunga lakini bibi yake aliyekuwa Burundi  amekuwa akimuombea kwa muda mrefu hasa katika mechi ya Simba na Yanga ili aweze kufunga hivyo bao alilofunga anamzawadia yeye.


“Nimefurahi sana kuona nimefanikiwa kufunga, bao la leo ambalo namzawadia  bibi yangu aliyeko Bunjumbura Burundi kwani amekuwa akinishauri vitu vingi juu ya kufunga na kuniombea niweze kufanikiwa kufunga hasa katika mechi hii dhidi ya Yanga, hivyo nimefurahi sana kuona nimefanikiwa kufunga.


“Mechi yetu na Yanga ilikuwa ngumu kwani kila upande ulikuwa ukihitaji kuibuka na ushindi, lakini kwa upande wetu tumefurahi kuona tumefanikiwa kushinda kwani ndio chachu ya sisi kuweza kufanya vizuri zaidi na kabla ya mchezo bibi aliniambia ananiombea nifunge.



“Nawaomba mashabiki wa Simba waweze kutusapoti na kutuombea ili tuweze kufanikiwa kuwapa kile kitu ambacho walikuwa hawakipati kwa muda mrefu, tunajipanga ili kuweza kutwaa ubingwa,” alisema Mavugo.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic