March 12, 2017


Hofu imeingia kwa kikosi cha Monaco ya Ufaransa, kwamba wanaweza kumkosa nahodha wao Radamel Falcao katika mechi dhidi ya Man City.

Man City itarudiana na Monaco katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 Bora.
Lakini Falcao alilazimika kwenda nje baada ya kuumia nyonga katika mechi ya Ligi Kuu Ufaransa maarufu kama League 1 dhidi Bordeaux.


Mechi hiyo ya marudiano itakayopigwa Jumatano ni muhimu sana kwa Monaco na inamhitaji Falcao ambaye alifunga katika mechi ya kwanza.
Hata hivyo, safe ya madaktari wa Monaco wamesema, watatoa taarifa baada ya kuanza matibabu na kuona. 
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV