March 12, 2017



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi kesho Jumatatu, Machi 13, 2017 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kufunga kozi ya ukocha ngazi ya ‘Intermidiate’ kwa makocha 27 wanaotarajiwa kuhitimu.


Kozi hiyo iliyoendeshwa na Wilfred Kidao - Mkufunzi anayetambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), itafungwa saa 5.00 asubuhi kwenye Viwanja vya Michezo vya Bandari, vilivyoko Tandika jijini Dar es Salaam.


Mbali ya Kidao, wakufunzi wengine walikuwa ni Manyika Peter aliyefundisha programu au mtaala kwa makocha wa makipa; Dk. Nassoro Ally Matunzya aliyewanoa makocha hao kuhusu tiba za wanamichezo/wanasoka na Mkufunzi wa muda mrefu wa soka, Hemed Mteza.


Wengine ni nyota wa zamani wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ waliopata kuchezea klabu kongwe na kubwa nchini. Wanafunzi hao ni Boniface Pawasa, Fred Mbuna, Innocent Haule, Herry Morris, Ivo Mapunda, Nizar Khalfan na Mussa Hassan Mgosi.


Wengine ni Omar Kapilima, Amosi Mgisa, Uhuru Mwambungu, Yussuf Macho, George Minja, Haruna Adolf, Selemani Omari, Ally Ruvu, Masoud Selemani, Haji Mustapha, Mhasham Khatib, Issa Ndunje, Salum Kapilima, Said Salum, Julio Elieza, Hassan Mwakami, Rajab Mponda, Ally Mbonde na Evod Mchemba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic