March 3, 2017

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amemrejesha kwenye kikosini beki wake, Luke Shaw katika orodha ya wachezaji ambao wanatarajiwa kuwemo kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Bournemouth katika Premier League.

Taarifa kutoka ndani ya Man United imethibitisha juu ya uamuzi huo wa Mourinho ikiwa ni baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mazoezi yaliyokuwa yakifanyika kwenye Uwanja wa Carrington.


 Beki huyo ambaye amekuwa kwenye kipindi kigumu kutokana na kutokuwa na uhakika wa kucheza, hajacheza katika Premier League tangu Oktoba ena ameanza mechi moja tu katika michuano yote msimu huu, katika mchezo dhidi ya Wigan kwenye FA Cup.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV