March 3, 2017






Na Saleh Ally
VINARA wa Ligi Kuu Bara kwa sasa ni kikosi cha Simba kinachoongozwa na Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon. Simba iko kileleni ikiwa na pointi 54.


Pamoja na kuwa kileleni, Simba ina presha kubwa kwa kuwa ni sawa na mtu aliyewahi kugongwa na nyoka. Hata ujani ukimgusa, hofu inasambaa.


Hii inatokana na kwamba, Simba iliongoza hadi tofauti ya pointi nane na timu iliyokuwa katika nafasi ya pili ambayo ni Yanga. Katika mechi mbili za mwisho wa mzunguko wa kwanza, ikaporomosha pointi sita baada ya kufungwa mechi mbili.


Baada ya kuanza kwa mzunguko wa pili, ikaendelea kuporomoka hadi Yanga ilipokaa kileleni. Simba imepambana tena na kurejea kileleni kwa mara nyingine. Uhakika wa kurejea ni baada ya kuifunga Yanga kwa mabao 2-1.


Kwa sasa Simba ina hofu na presha. Inachotaka ni kuendelea kushinda na moja ya mambo imefanya ni kumuomba au kumuangukia beki wake, Juuko Murshid arejee na kujiunga nao.


Murshid anarejea kujiunga na Simba tangu alipokwenda katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) ambayo sasa ni zaidi ya mwezi mmoja tangu iishe. Ninakumbuka alipata msiba wa kufiwa na wanaye, hakika nampa pole kubwa na kumpa moyo kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayepanga na anajua alichomuandalia.


Lakini naendelea kusisitiza, alipaswa kukumbuka umuhimu wa Simba iliyompa muda wa kupumzika na pia kuungana na familia yake baada ya matatizo.


Maana alianza kuonyesha dharau kwa vile ana nafasi ya kwenda nje lakini amesahau Simba ilimpa nafasi ya kucheza timu ya taifa na sasa anakwenda kucheza Ulaya.


Uongozi wa Simba, umelazimika kufanya kazi ya ziada ikiwa ni pamoja na kumbembeleza Juuko arejee kuisaidia Simba kwa kuwa imebanwa.


Beki tegemeo wa kati, Method Mwanjale ni majeruhi, Novaty Lufunga ana kadi tatu za njano na Besala Boukungu ambaye angeweza kuziba pengo ana adhabu ya kadi nyekundu. Sasa anabaki Abdi Banda pekee ambaye yuko fiti.


Simba haina ujanja, hata kama iliamua kumuacha Juuko aendelee kuidengulia, inaamua kurudi na kuanza kumbembeleza upya ili arudi na “kuisaidia” tena Simba ambayo kwa haki bin haki, haikupaswa kuwa hivyo.


Juuko ni mchezaji wa kulipwa, aliyepewa nafasi na Simba hadi akapata nafasi ya uhakika timu ya taifa ya Uganda na baadaye kuonekana na sasa anakwenda kucheza Ulaya. 


Hata kama nafasi kwake imekuwa nzuri The Cranes kwa kuwa kuna mkono wa Kocha Sredojevic Milutin ‘Micho’ lakini hawezi kukwepa heshima au shukurani kwa Simba.


Alibaki Uganda hadi wiki iliyopita kwa nini hasa? Hajui Simba inapambana kuwania ubingwa na inahitaji huduma yake kwa kuwa jina lake linaendelea kujaza idadi ya wageni pia wachezaji waliosajiliwa kihalali.


Juuko alionyesha dharau kwa Simba kwa kuwa ni ya Tanzania ambako ni jirani na kwao? Anaweza kufanya dharau hizo huko aendako sasa? Au atakuwa mwoga kwa kuwa ni kwa Wazungu?


Lakini inawezekana amefanya dharau kwa kuwa viongozi wa Simba nao si imara kwa kuwa wanaogopa kumkorofisha ni kuwaudhi mashabiki? Kama ni hivyo, basi si sahihi hata kidogo na ubora wa uongozi ni kusimamia vilivyo sahihi.


Juuko ana mchango wake Simba, lakini aliondoka na Simba ikaendelea kushinda. Amerudi ameikuta kileleni. Hivyo anapaswa kuonyesha nidhamu na lazima ajue hata kama ni bora vipi anapaswa kuheshimu utaratibu sahihi.


Kuidharau Simba ni kuwadharau vongozi, wachezaji wenzake na mashabiki. Alichofanya Juuko hata kama viongozi Simba wanakificha, mimi nasema haikuwa sawa na viongozi hawapaswi kuwaachia wachezaji wengine wawe juu ya sheria wakati wengine wanaheshima na kuzifuata. Hili la Juuko, liwe la mwisho Simba ni kubwa kuliko kila mmoja aliye ndani yake.


SOURCE: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Kaka simba sio mara ya kwanza kusujudia wachezaji hasa wa uganda, kuna mtu hata leo akisema anataka millioni 100 kusajili kwa mwaka watampa si mwingine ni Okwi na amini nakwambia leo mwakani Okwi atacheza simba. Nadhani tatizo lipo ktk mikataba, mbona ulaya mchezaji akichelewa kureport anakatwa mshahara na adhabu nyingine? Kwanini huku ni ufala ndio unaendelea.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ww salehe ally ni Yanga damu sasa kimewauma kuona juko karudi unadhani ile mechi ya yanga angecheza juko mnepata ata goli la offside? pilipili ya shamba inawawashia nn mbona nyie manji alikua akisusa kidogo hadi mnampigia magoti? fanyeni yenu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic