Mshambuliaji mkongwe wa Atletico Madrid, Fernando Torres ameumia vibaya na kusababisha kutolewa kwa gari la wagonjwa na kukimbizwa hospitali akiwa ameishapotea fahamu.
Torres aliumia wakati akiwania mpira na beki wa Derpotivo La Coruna katika mechi iliyoisha kwa sare ya bao 1-1, jana.
Hata hivyo, taarifa zilizotolewa asubuhi zimeeleza, Torres yuko vizuri naye alitupia mtandaoni kuwashukuru mashabiki waliomuombea.
0 COMMENTS:
Post a Comment