March 29, 2017Mmoja wa wachezaji gwiji waliowahi  kutokea nchini Brazil, Ronaldinho rasmi ameingia kwenye muziki.

Ronaldinho aliyestaafu mwaka 2015, ameibuka na sing mpya aliyoipa nina la ‘Sozinho’.

Mkali huyo aliyewahi kung’ara akiwa Barcelona, sasa ana umri wa miaka 37 lakini ameamua kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanamuziki.


Muziki wake ni katika miondoko ya Samba ambayo ni maarufu nchini Brazil na kama unakumbuka, Ronaldinho mara kadhaa alikuwa akitoroka Barcelona au wakati yupo PSG kwenda kuhudhuria tamasha la muziki wa Samba, kwao Brazil.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV