March 5, 2017Mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta ameendelea kuonyesha ni mtu “hatari” baada ya kufunga mabao mawili wakati timu yake ya Genk ikishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Club Brugge.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Ubelgiji, wageni Brugge walionekana ni hatari dakika za mwanzo, lakini dakika ya 5 tu, Samatta akawatuliza kwa kufunga bao la kwanza akipokea pasi ya Ruslan Malinovsky.


Samatta alirejea tena kambani katika dakika ya 42 akifunga baada ya kupokea pasi ya Pozuelo na Brugge wakafunga bao lao pekee dakika ya 43 kupitiaJose Izquierdo.

Nahodha huyo wa Taifa Stars, alipumzishwa katika dakika ya 85 baada ya kuwa amemaliza kazi yake hiyo muhimu


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV