March 17, 2017


Mchana huu ndiyo siku ambayo tunaweza kupata jibu kama KRC Genk ya Mbwana Samatta inaweza kuivaa Man United?

Timu zote mbili zimeingia katika robo fainali ya Europa League.

Katika shughuli ya upangaji ratiba ya robo fainali itakayofanyika Nyon, Uswiss, leo mchana. Huenda lolote linaweza kutokea.

Kama Genk itapangwa na Man United, basi kitakuwa kipimo kingine kwa Samatta kuonyesha ubora wake.

Hata hivyo kuna timu nyingine kubwa kama Ajax, Lyon, Schalke, Celta Vigo na wababe wa Ubelgiji Anderlecht ambao kama wakipangwa na Genk, Samatta atapata nafasi ya kuonyesha yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV