March 23, 2017


Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Tong Gang akizungumza na wageni waalikwa.

Kampuni ya StarTimes Tanzania, jana Jumatano iliwakutanisha Watanzania na Wachina katika kusherehekea Wiki ya Filamu za China kwenye hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Quality Center jijini Dar.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wasanii kutoka Tanzania na China, mgeni rasmi alikuwa Nape Nnauye ambaye awali alikuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, kabla ya kutenguliwa uteuzi wake.

Tong Gang (wa tatu kutoka kushoto) akikata utepe

“Wachina ni ndugu zetu na hatuna budi kujumuika nao katika kusherehekea Wiki ya Filamu za China ambapo ni furaha kwetu kuona baadhi yao wakijua kuzungumza Kiswahili.

“Tunachotaka kufanya sasa ni kuzitafsiri filamu za Kitanzania kwa Lugha ya Kichina ili ndugu zetu hawa waweze kuziangalia kule kwao kama ilivyo kwa filamu zao zilizotafsiriwa kwa Kiswahili,” alisema Nape.Naye Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Tong Gang, alisema: “NI faraja kwetu kuona tunadumisha undugu ambao ulianzishwa na babu zetu huko nyuma, sisi kama warithi tunapaswa kuuendeleza na kwa kupitia filamu naamini tutafanikisha hilo.”
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV