March 10, 2017


Mshambuliaji nyota Mtanzania, Mbwana Samatta ameonyesha kweli ni moto baada ya kufunga mabao mawili wakati timu yake ikishinda kwa mabao 5-2 ugenini dhidi ya Gent.

Genk imeichapa Gent, zote za Ubelgiji kwa mabao 5-2 katika mechi ya raundi ya 16 Bora Europa Cup, kuwania kwenda robo fainali.

Samatta ambaye watangazaji wengi wa runinga barani Ulaya wamekuwa wakitamka jina lake “Bwana Samatta”, alianza kufunga katika dakika ya dakika ya 41, likiwa bao la tatu.

Kabla Ruslan Malinovsky alikuwa amefunga bao kwa mkwaju wa adhabu katika dakika ya 21 na Gent wakasawaisha kupitia kinda Mnigeria, Samuel Kalu katika dakika ya 27.

Omar Colley raia wa Gambia akaongeza bao la pili dakika ya 33 kabla ya Samatta kufunga na Jere Uronen akafunga la nne kabla ya kwenda mapumziko.

Gent ambao walikuwa nyumbani walianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 61 kupitia Kalifa Coulibaly.

Wakati Gent wanaona mambo yanaenda vizuri, Genk wakaamka na Samatta akapigilia msumari wa tano katika dakika ya 72 akiunganisha krosi safi ya Thomas Bufel.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic