March 23, 2017Yanga wataendelea na mazoezi leo kujifua kujiandaa na mechi za nyumbani na kimataifa.

Kikosi hicho chini ya George Lwandamina raia wa Zambia, kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Yanga inaendelea kujifua kwa kuwa pamoja na Ligi Kuu Bara, wanatakiwa kuendelea kuwa fiti kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema wachezaji wako katika hali nzuri.

“Mazoezi ni kawaida ya kuendelea kujiweka vizuri lakini wachezaji wako vizuri,” alisema.


Yanga imekuwa na msimu bora kabisa katika msimu uliopita lakini tofauti na msimu huu, inaonekana mambo hayajakaa vizuri sana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV