Kama unakumbuka, Masau Bwire alisema watawazika Yanga baada ya kuuwawa na Mnyama Simba, mambo yamegeuka.
Lakini mambo yamegeuka leo na Yanga ndiyo wamewazika Ruvu Shooting na kuwachapa kwa mabao 2-0.
Pamoja na Yanga kuwa pungufu baada ya Obey Chirwa kutolewa kwa kadi nyekundu. Bado iliweza kupata bao dakika ya 90 kupitia kwa Emmamuel Martin na kushinda kwa 2-0.
Kabla, Simon Msuva alikuwa ameandika bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti.
Yanga inaendelea kubaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 52 nyuma ya watani wao Simba, vinara wa Ligi Kuu Bara wenye pointi 54.
0 COMMENTS:
Post a Comment