GOOOOOOOO krosi safi ya Msuva, Martin anaruka juu kama kishada na kuandika bao safi la pili kwa Yanga kwa kichwa
-Ruvu wanaonekana hawana mpango mbadala zaidi ya kusubiri mechi iisheee
-Hakuna mashambulizi makali upande wowote na Yanga wanazidi kuwapunguza kasi Ruvu
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90, Ruvu wanapata kona, inachongwa, hatariiii, Maganga anagonga kichwa lakini Dida anadaka kwa ustadi kabisa
Dk 89 sasa kinachoonekana sasa ni Yanga wanalinda lango lao kuhakikisha wanapata ushindiKADI Dk 85 Kessy naye analambwa kadi ya njano kwa kucheza kindava hapa
KADI Dk 83 Madega analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Martin
Dk 80, Mwinyi Haji anaachia mkwaju mkali kabisa anaokoa na kuwa kona. Inachongwa, anaokoa tena inakuwa kona nyingine
Dk 79 Kisiga anaenda nje na nafasi yake inachukliwa na Mtuwi
SUB Dk 77, Yanga wanawatoa Deus Kaseke na Justine Zulu na nafasi zao zinachukuliwa na Juma Mahadhi na Martin Emmanuel
Dk 76 sasa, hakuna tofauti inayoonekana kuwa Yanga wako pungufu mtu mmoja na Ruvu hawaonyeshi kuitumia nafasi hiyo
Dk 72, Maganga anawachambua mabeki watatu wa Yanga lakini mkwaju wake, unakuwa nyanya mikononi mwa Dida
Dk 69 sasa, Yanga wanapoteza nafasi nyingine nzuri baada ya kubaki wawili kwa wawili lakini Msuva anakuwa na papara na mabeki Ruvu wanaokoa
Dk 64 krosi nzuri kabisa hapa lakini shuti linatoka sentimeta chache kwenye lango la Ruvu
SUB Dk 63, Yanga wanamtoa Mwashiuya na nafasi yake inachukuliwa na Said Juma MakapuDk 63, Yanga wanapata kona baada ya shambulizi jingine
Dk 62, Yanga wanafanya shambulizi jingine, shuti la Kessy linatoka sentimeta chache kabisa
Dk 59 sasa Ruvu wanaonekana kupata uhai na kuonana vizuri kuliko awali
Dk 57, Ruvu wanaingia vizuri na Maganga Fullzuri aaanachia mkwaju lakini unatoka na kupiga nyavu ndogo
Dk 57, nafasi nyingine nzuri kwa Yanga, Tambwe katika nafasi nzuri anaachia mkwaju, kipa anaokoa
Dk 55, Mwashiuya anaingia vizuri na kuachia mkwaju matata hapa lakini ni goal kick
Dk 53, Msuva anammegea pasi nzuri Mwahiuya lakini krosi yake haikufika alipo Tambwe
Dk 51, Yanga wanapata kona, inachongwa na Msuva lakini inaokolewa kiulaini kabisa
Dk 51, Msuva anajaribu shuti la mbali lakini mpira unatoka nje kidogooo
SUB Dk 49 Chande Magoja anakwenda nje anaingia Shaaban Msala upande wa Ruvu
DK 48 Tambwe anaukwamisha mpira wavuni hapa lakini mwamuzi msaidizi anasema ni offside
Dk 47, krosi safi ya Haji Mwinyi ndani ya lango la Ruvu Shooting lakini wanaokoa
DK 45 Yanga wanaonekana kuanza kwa kasi wakiwa wamepania kupata bao la pili. Kumbuka wako pungufu mtu mmoja
MAPUMZIKO
45+2 Yanga wanapata kona, inachongwa na kuokolewa, kona tena. Inachongwa hapa lakini haina mashara
KADI Dk 45, Chirwa analambwa kadi ya njano ya pili kwa kupiga mpira chini kwa nguvu, inazaa KADI NYEKUNDU
KADI Dk 44, Chirwa anaupachika mpira wavuni kwa kichwa lakini mwamuzi anamlamba kadi ya njano kwa kuwa alishika kabla ya kufunga, LAKINI PICHA ZINAONYESHA HAKUSHIKA
Dk 43 Bossou anajaribu mkwaju wa faulo lakini unapita juu ya lango la Ruvu
Dk 41, Kanduru wa Ruvu analala chini, inaonekana aligongwa tumboni na Cannavaro wakati akiokoa
Dk 40, Msuva anaangushwa ndani ya eneo la hatari.
Mwamuzi anasema boli liendeleee, Msuva anaonekana kulaumu hapa
Dk 37 kipa JKT anafanya maajabu tena, anaokoa akiwa amebaki yeye na Mwashiuya
Dk 37, Mguya anapiga shuti kali kabisa lakini hakulenga
Dk 34, Kisiga aanachia mkwaju matata kabisa wa adhabu, Dida anapangua na kuwa kona. Inachongwa, inaokolewa na kuwa goal kick
KADI Dk 33, Cannavaro analambwa kadi ya njano
GOOOOOOOOOOOOOOOOOO DK 31 Msuva anafunga vizuri kabisa hapaaa
DK 30, Chirwaa anaachia mkwaju mkali lakini mwamuzini anasema Mayoka ameunawa. Ni PENAAAAAAT
Dk 26, mpira wa kona, Bossou kabaki yeye na lango lakini anapaisha, juuuuu. Kipa Hussein yuko chini anatibiwa
Dk 25, Chirwa anamtoka Makwaya anabaki yeye na kipa, lakini kipa anaokoa na kuwa kona
DK 25, Yusuf Mguya anaachia mkwaju mkali lakini hakulenga lango
Dk 22, Yanga wanapata kona tena baada ya beki Mwakwaya kuuwahi mpira wa Mwashiuya, inachongwa lakini gial kick
Dk 20, Kessy anaingia vizuri na kutoa pasi nzuri kabisa kwa Chirwa lakini anashindwa kuumiliki mpira, unaokolewa
Dk 19, krosi ya Mwinyi lakini anashindwa kulenga lango
Dk 15, Ruvu Shooting nao wanaonekana kucharuka, wanagongeana vizuri lakini hakuna mashambulizi makali sana
Dk 12, Kipa Ruvu, Muhidin Hussein anatokea na kuokoa vizuri hapa, lakini yuko chini anaonekana ameumia na daktari anaingia kumtibu
Dk 11, Kaseke anaingia vizuri lakini mkwaju wake unazuiliwa wa kuwa kona
Dk 10, Kessy aaaachia mkwaju mkali kabisa unagonga mwamba na kurejea uwanjani lakini unaokolewa hapa
Dk 9, Damas Makwaya anafanya ziada na kuutoa mpira unakuwa kona ya kwanza ya mchezo huu. Unapigwa kwenye lango la Ruvu, wanaokoa
Dk 6, Almanusura Tambwe auwani mpira na kupachika wavuni, lakini kipa wa Ruvu anafanya kazi nzuri kabisa
Dk 4, uzembe wa Bossou, anachinganya na Kisiga anaachia mkwaju mkali na unatoka sentimeta chache nje ya lango la Yanga
Dk 3, mabeki wa mabeki wa Ruvu wanafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mbele ya Mwashiuya
Dk 3, krosi nzuri kwenye lango la Yanga lakini Cannavaro anaruka na kuokoa vizuri
Dk 1, mechi imeanza na Yanga ni wa kwanza kufika lango la Ruvu
0 COMMENTS:
Post a Comment