April 20, 2017


Baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga ngumi nahodha wa Kagera Sugar, George Kavila na kufungiwa mechi mbili, beki Abdi Banda wa Simba, sasa yuko tayari kucheza mechi zilizobaki za Simba.

Banda ana nafasi ya kucheza mechi zote tatu dhidi ya African Lyon, Stand United na Mwadui.

Hii inatokana kwamba, kabla ya kufungiwa alitakiwa kutocheza hadi uchunguzi ufanyike, hivyo akakosa mechi mbili kwenye Uwnaja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Simba ilipoivaa Mbao FC na Toto African.

Baada ya kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji kumfungia mechi mbili, maana yake tayari ameishaitumikia adhabu hiyo.


Hivyo atakuwa huru kuitumikia Simba katika mechi tatu zilizobaki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV